Siku chache zilizopita, Haji S Manara aliachana na mke wake Zaiylisa. Sababu kubwa ya kuachana kwao Manara alidai kuwa mrembo huyo hakuwa anaishi vizuri na watoto wake, huku Zaiylisa akikanusha madai hayo na kusema kuwa kuna mambo mengine ya siri ambayo yamewaachanisha kwani zama za sasa sio zakunyanyasa watoto.


Lakini tarehe 19 Aprili 2025, Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram alipost video akiwa na mrembo mpya. Video hiyo iliyomuonesha akiwa na mpenzi wake mpya iliisindikiza kwa maneno yaliyosema, “Muda wa kuanza maisha mapya”.


Hapo alionekana akiwa na mwanamke ambaye hakumuonesha Sura, lakini alionesha ameshamvalisha Pete, mbali na apo walionekana wakifurahi pamoja kwa kunywa, kukumbatiana na kutembea pamoja.


Video ya majara imewashangaza watu wengi sana maarufu kama na wengine wengi ambao wameonekana kushangazwa na kitendo cha Manara kuoa haraka hivyo. Lakini pia wengine wamefurahi kwa kuona Haji Manara anapata wakumfariji.

Facebook Comments Box