Hii ni moja ya matukio yaliyozua gumzo kubwa mitandaoni! Msemaji wa Chama cha National Unity Platform (NUP), Alex Waiswa Mufumbiro, ameandika historia ya kipekee baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Nakawa Mashariki, licha ya kuwa bado yuko gerezani.

Alex Waiswa alikamatwa mwaka 2025 nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kawempe, jijini Kampala, alipokuwa ameenda kushuhudia kesi ya Eddie Mutwe, ambaye anajulikana kama mkuu wa ulinzi wa kiongozi wa NUP, Bobi Wine. Tukio hilo lilizua mijadala mikali mitandaoni, huku wengi wakishangazwa na hatua hiyo.
Baada ya kukamatwa, Alex Waiswa aliunganishwa katika kesi moja na Eddie Mutwe, na wote wawili wakapelekwa Gereza la Luzira, Kampala. Hadi sasa, amedaiwa kuwa amekaa gerezani kwa zaidi ya siku 78 bila kuachiwa huru.

Kinachovutia zaidi ni kwamba, licha ya kuwa nyuma ya vyuma, wakazi wa Nakawa Mashariki bado walimchagua Alex Waiswa kuwa mbunge wao kupitia NUP. Ushindi huo umeibua gumzo kubwa mitaani na mitandaoni, huku wengi wakisema ni “kura ya hisia” na wengine wakitafsiri kama ujumbe mzito kwa uongozi wa nchi.
Je, huu ni mwanzo wa ukurasa mpya wa siasa za Uganda au ni tukio jingine linaloonyesha nguvu ya umaarufu? Muda ndio utakaoamua… 🔥



