Thursday, December 18, 2025
spot_img
HomePoliticsKutoka utii hadi tahadhari: kuusoma ukimya wa leo Tanzania.”

Kutoka utii hadi tahadhari: kuusoma ukimya wa leo Tanzania.”

Dar leo iko kimya — kimya ambacho hakijazoeleka. Kwa hali ilivyo jijini Dar es Salaam, inaonekana watu wametii agizo la kukaa ndani… au tuache masihara, wanaogopa.               Mitaa ambayo kawaida huwa na shughuli nyingi leo inaonekana kimya kuliko kawaida, hali inayoashiria kuwa hatua za serikali zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kudhibiti mwitikio wa wananchi.

Hatua ya kufungia akaunti za wanaharakati na kupunguza njia za kupaza sauti imeleta athari inayoonekana: watu kukosa majukwaa ya kuhamasishana. Hata hivyo, swali muhimu linabaki: Je, wananchi wametii kwa hiari ili kulinda amani, au wamelazimika kubaki ndani kutokana na hofu ya kukamatwa, kufuatiliwa, au kudhibiwa? Hili ndilo jaribio halisi la kutathmini uhusiano kati ya dola na raia wake katika kipindi hiki cha msukosuko wa kisiasa.

Serikali ilipofungia akaunti za wanaharakati na kuzima sauti za mitandaoni, walijua wanachofanya: kukata mikono na miguu ya harakati za wananchi. Na matokeo yake tunaona leo — mitaa imepoa, sauti zimenyamaa, presha imeshuka. Lakini swali bado linawaka kama moto: Je, Watanzania wametii kwa hiari… au wameteleza kimya kimya kwenye hofu? Utii unaotokana na hofu si utii — ni kimya cha kulazimishwa. Na kimya cha kulazimishwa huwa hakidumu.

Facebook Comments Box
RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -spot_img

Most Popular

Recent Comments