Saturday, November 22, 2025
spot_img
HomeCrimeTaarifa Mpya Kuhusu Kifo cha MC Pilipili: Familia Yadai Kulikuwa na Matukio...

Taarifa Mpya Kuhusu Kifo cha MC Pilipili: Familia Yadai Kulikuwa na Matukio ya Kutatanisha Kabla ya Kifo

Dodoma — Taarifa mpya kutoka kwa baadhi ya ndugu na watu wa karibu wa MC Pilipili zimeibua maswali mapya kuhusu mazingira yaliyopelekea kifo cha msanii huyo, ambaye mwili wake ulipatikana Jumapili, Novemba 16, 2025 katika eneo la barabara ya Dodoma.

Kulingana na taarifa ambazo familia inadai ilizipokea, Marehemu MC Pilipili alionekana kwa mara ya mwisho Jumamosi Novemba 15, mara baada ya kusafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa shughuli zake binafsi.

Tukio la Siku ya Jumapili

Siku ya tukio, inadaiwa kuwa MC Pilipili aliondoka katika Royal Village Hotel, na wakati akiondoka, kulikuwa na magari mawili yaliyodaiwa kumfuata kwa karibu. Mashuhuda wanaripoti kuwa magari hayo yaliendelea kumfuatilia hadi maeneo ya karibu na Swaswa, Dodoma mjini.

Mashuhuda hao wanadai kuwa kulitokea ubishani wa muda mfupi kati ya MC Pilipili na watu waliokuwa kwenye magari hayo. Inasemekana kuwa baadaye alishushwa kwa nguvu kutoka kwenye gari lake na kuingizwa katika gari jingine.

                           

Kupatikana kwa Mwili

Familia iliarifiwa baadaye kuwa mwili wa MC Pilipili ulikuwa umeokotwa kando ya barabara, na tayari umefikishwa katika General Hospital, Dodoma. Ndugu walipofika hospitalini na kukagua mwili, wanadai kuwa waliona majeraha kadhaa ikiwemo:

  • Jeraha linalofanana na jeraha la risasi

  • Alama zinazoonekana kama za fimbo au mijeledi mgongoni

  • Alama zinazodaiwa kuashiria kuchomwa na kitu chenye joto

Kwa mujibu wa familia, alama hizo “zinaashiria uwezekano wa marehemu kupitia mateso kabla ya kifo,” ingawa hakuna uthibitisho rasmi kutoka kwa mamlaka za usalama.

Ukimya wa Mamlaka

Familia imesema imeelezwa kutotoa kauli yoyote kwa umma, na kwamba taarifa rasmi “zitatolewa na RPC wa Dodoma.” Hadi sasa, vyombo vya usalama vijatoa taarifa ya kina kuhusu uchunguzi wa tukio hilo.

Wananchi na wadau wa sanaa wameendelea kutaka uchunguzi wa kina na uwazi ili kufahamu kilichotokea siku ya tukio, huku kukiwa na wito wa kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa iwapo kutathibitika kuwepo kwa uhalifu.

Facebook Comments Box
RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -spot_img

Most Popular

Recent Comments